Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30 ameuawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kukamatwa na pikipiki ya wizi Katika kijiji cha kagongwa Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa nane Mchana mara baada ya marehemu kuiba Pikipiki hiyo yenye no T634 CNK Aina ya SanLG mali ya Patrick Seba mkazi wa Nyahanga Mjini Kahama ambayo imeibiwa jana Asubuhi Maeneo ya shule ya Kahama Musilim ikiwa imeegeshwa na dereva wake aitwaye Shija Zacharia.
Kwa mujibu wa Mmiliki wa pikipiki hiyo Bwana Seba Ameiambia redio Kahama fm Kuwa alipewa taarifa na dereva wake ambpo aliamua kutoa tarifa ya upoteza pikipiki hiyo kwa waendesha bodaboda wa mjini Kahama na Kagongwa.
0 comments:
Chapisha Maoni