Jumatatu, Machi 24, 2014

HABARI KAMILI KUHUSU NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA...IMEZAMA KATIKA BAHARI YA HINDI NA HAKUNA ALIYENISURIKA


Ndege iliyopotea
WAZIRI Mkuu wa Malaysia, Najib Razak ametangaza habari mpya kwamba ndege ya abiria iliyopotea ilimalizia safari yake kusini mwa bahari ya Hindi, tangazo ambalo limewavunja moyo wanandugu wa abiria.
Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Razak akitangaza leo juu ya utafiti wa rada kuonyesha kuwa ndege iliyopotea imeangukia katika bahari ya Hindi.
Ndege hiyo ya abiria ya Malaysia iliyokuwa na namba MH370 ilitoweka katika rada za kiraia saa moja baada ya kuruka kutoka Kuala Lumpur kuelekea  Beijing ikiwa na watu 239 ndani yake hapo Machi 8 mwaka huu.
Ndege ya majini toka Australia ikielekea eneo ndege ya Malaysia ilipodondokea
Kutokana na vipimo vyo radar, hapa ndipo ndege ilipodondokea
Hakuna habari zilizothibitishwa juu ya kuonekana kwa mabaki ya ndege hiyo, ingawa kumekuwa na vitu vinavyoonekana huko pwani ya Australia vinavyodhaniwa huenda ni sehemu ya chombo hicho. Ndugu wa abiria waliokuwemo ndani, wameanza mipango ya kusafiri kuelekea huko.
Wanajeshi wa jeshi la Australia wakiwa ndani ya ndege katika kituo cha Kijeshi cha AP-3C Orion.
Hata hivyo, vitu vilivyoonekana kwenye satellite ya China na Ufaransa, bado havijaweza kufikiwa na kutambuliwa kama vina uhusiano wowote na ndege hiyo ambayo ni gumzo kwa sasa duniani.

0 comments:

Chapisha Maoni