Manchester United imepokea kipigo cha bao 3-0 kutoka kwa Manchester
City katika mechi ya Ligi Kuu England iliyopigwa Uwanja wa Old Trafford
jijini Manchester hivi punde.
Wafungaji katika mechi ya leo ni Edin Dzeko aliyefunga mabao mawili
dakika ya 1 na 56 la tatu likifungwa na Yaya Toure dakika ya 90.
Kwa matokeo ya leo, Manchester City wamepanda mpaka nafasi ya pili
wakati Manchester United wakiwa nafasi yao ya saba katika msimamo wa
ligi hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni