Ijumaa, Machi 28, 2014

KAJALA AMFANYIA WEMA UMAFIA, ANUNULIWA GARI NA YULE KIGOGO WA IKULU WA WEMA


NI madai mazito! Kwamba, nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja amehongwa gari na mtu anayedaiwa kuwa ni kigogo wa Ikulu.
Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zipo hadi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram, Kajala alinunuliwa gari hilo aina ya Toyota Brevis lenye rangi ya bluu iliyoiva  wiki mbili zilizopita mara baada ya kutua Bongo akitokea nchini China ambako alikwenda kwa mambo yake binafsi.
Wasambaza taarifa hao walidai kuwa, kigogo huyo wa Ikulu ni yule Clement ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.
“Mmeisikia hii? Kajala amenunuliwa gari na Kile (Clement), lina thamani ya shilingi milioni kumi na moja, Wema alie tu nakwambia. We ukisema cha nini wenzako wanajiuliza watakipata lini?
KAJALA MASANJA
 “Kwanza mnajua kama bifu la Wema na Kajala lilitokana na Clement? Alipoachana na Wema akatua kwa msichana anaitwa Naima, lakini akaona bado akaenda hadi kwa Kajala. Wema alipogundua ndiyo akamnunia na kuanza ushoga na Aunt Ezekiel,”Kilidai chanzo.
GARI ALILONUNULIWA KAJALA
Awali, mtoa habari mmoja alisema Kajala yupo na gari hilo Kinondoni kwa Manyanya, lakini alipofuatwa hapo hakuonekana.
Habari zikapatikana kwamba, alikuwa kwenye Mgahawa wa Steers uliopo jengo la Millennium Tower, lakini pia alipofuatwa eneo hilo hakuonekana.
Kuhusu kufa kwa ushoga wao, awali Kajala hakutaka kulizungumzia suala hilo lakini alipobanwa alidai hana tatizo na Wema na kwamba kwa sasa yuko bize kutengeneza filamu zake.
Kwa upande wake, Wema alipopigiwa simu hakupokea lakini siku za nyuma aliwahi kuanika kwamba haamini kama Kajala anaweza kutembea na Clement. Hapo ni wakati ule wakiwa mashoga.

0 comments:

Chapisha Maoni