Ndege na meli kutoka nchi mbali mbali zinaendelea
kuitafuta mabaki ambayo huenda yanatokana na ndege ya Malaysia
iliyopotea takriban wiki mbili zilizopita ikiwa imebeba takriban watu
240.
Matumaini ya kutatua kitendawili hicho
yaliongezeka baada ya Australia kutoa picha za Satelaiti za vitu viwili
vilivyoonekana baharini vuikidhaniwa kuwa vifusi vya ndege hiyo.
Hata hivyo hadi kufikia sasa hakuna cha maana kilichopatikana.
Afisa mmoja mkuu wa New Zealand amesema operesheni hiyo ilitatizwa na kuchafuka kwa bahari na kutoona vizuri.
Meli ya mizigo ya Norway ilitumia taa kuyatafuta mabaki hayo pasina kufanikiwa.
0 comments:
Chapisha Maoni