MSANII wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ ametoa kali ya mwaka
baada ya kusema kuwa hayupo tayari kuolewa na mwanaume mwingine zaidi
ya mkali wa Bongo Fleva, Ruta Maxmilian Bushoke aliyeko Afrika Kusini.
Akipiga stori na gazeti hili, Kabula alisema: “Ndoa yangu itakuwa na
Bushoke tu. Sijali umbali wetu, lakini naamini siku moja atakuja na
atanioa. Uhusiano wetu uko poa na tunawasiliana vizuri kila wakati,”
alisema Kabula na kuongeza:
“Siwezi kusema atakuja lini lakini nawaambia kabisa wanaonizengea,
watafute kitu kingine cha kufanya, mimi na Bushoke kilichobaki ni ndoa
tu.”
0 comments:
Chapisha Maoni