Kama unalikumbuka Ghorofa lililowahi kuingia kwenye list ya matukio makubwa kwa kuporomoka likiwa bado linaendelea na ujenzi sasa jana Mkurugenzi wa zamani wa Manispaa ya Ilala Gabriel Fuime na wenzake 11 wamesomewa upya mashtaka 27 ya mauaji katika ajali ya kuporomoka kwa jengo hilo la ghorofa 16 Dar.
Mkurugenzi huyo wa Mashitaka Nchini (DPP) amemfutia mashitaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Gabriel Fuime (61) na kisha kumuunganisha na wenzake 11 na kuwasomea upya mashtaka 27 ya mauaji yaliyotokea katika mtaa wa Indira Gandh yaliyosababishwa na kuporomoka kwa Ghorofa hilo.
Mbali na Fuime washtakiwa wengine ni Diwani wa Kata ya Goba Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki,Raza Ladha,Goodluck Mbanga,Willbroad Mugyabuso,Mohamed Abdulkarim,Charles Ogare,Zonazea Oushoudada,Vedasto Ruhale,Michael Hema,Albert Mnuo na Joseph Ringo.
Washtakiwa hao wamesomewa hati mpya ya mashitaka baada ya kuondolewa hati ya zamani ya mauaji ya bila kukusudiwa na kuunganishwa Fuime na idadi yao kufikia 12 mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka.
Washtakiwa hao wamesomewa hati mpya ya mashitaka baada ya kuondolewa hati ya zamani ya mauaji ya bila kukusudiwa na kuunganishwa Fuime na idadi yao kufikia 12 mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu,Benard Kongola akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi,Tumaini Kweka na Wakili wa Serikali Joseph Maugo.
0 comments:
Chapisha Maoni