Alhamisi, Machi 20, 2014

BOKO HARAM WATAKIWA KUSHUSHA SILAHA ZAO CHINI

Jeshi la Nigeria limelitaka kundi la Boko Haram liweke silaha chini na kufanya mazungumzo na serikali.
Kenneth Minimal Mkuu wa vikosi vya jeshi la Nigeria amesema, mazungumzo ndio chaguo bora kwa ajili ya kuhitimisha mapigano na kundi la Boko Haram na amelitaka kundi hilo kuweka silaha chini na kuketi katika meza ya mazungumzo na serikali ya Abuja.
Minimal amesema hayo alipotembelea mji wa Maiduguri kwenye eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria kunakohesabiwa kuwa ngome ya Boko Haram akiongozana na Kamanda wa Kikosi cha Anga cha nchi hiyo Adesola Mmusu. Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Nigeria amesema, jeshi limelitia kundi la Boko Haram hasara kubwa na kuwaua wafuasi wa kundi hilo. Amesema kundi hilo linapaswa kuelewa kuwa chaguo bora ni kuweka silaha chini na kuanza mazungumzo na serikali.

0 comments:

Chapisha Maoni