Mastaa wawili, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ na Rose Ndauka wamedaiwa kuwa
kwenye bifu chanzo kikidaiwa ni Rose kumtibulia mwenzake dili la ile
project ya kusafisha jiji iliyofanyika hivi karibuni.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake, chanzo
kilisema, wazo la project ile alikuwa nalo Batuli lakini Rose akaingilia
kati, hali iliyosababisha Batuli amnunie mwenzake.
Alipopigiwa Batuli kwanza aling’aka lakini akasema hapendi kuzungumzia
mambo hayo kwani yameshapita huku Rose akieleza kuwa, wazo la project
hiyo alikuwa nalo kabla hajajifungua hivyo haoni kama kamtibulia Batuli
dili lake.
0 comments:
Chapisha Maoni