Jumamosi, Februari 01, 2014

KOCHA ALIYEIPA UBIGWA HISPANIA AMEFARIKI DUNIA


Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania Luis Aragones amefariki dunia, akiwa na miaka 75, jumamosi ya leo katika clinic moja jijini Madrid, daktari Pedro Guillen amethibitisha.
Kocha huyu atakumbukwa kwa kuiongoza Hispania katika awamu mpya ya mafanikio mnamo mwaka 2008, alipoiwezesha timu hiyo kutwaa kombe la EURO na baada ya hapo alistaafu na kumpisha Del Bosque. Aliifundisha Spain kuanzia mwaka 2004 - 2008.

0 comments:

Chapisha Maoni