MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayeunda kundi la Makomandoo Fredy
Wayne ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na Jacqueline Wolper amesema
ameachana naye na sasa yupo na nyota mwingine wa filamu, Kajala Masanja.
Akizungumza FC hivi karibuni, Fredy alisema msanii huyo amemchanganya
mno kimapenzi kiasi kwamba ameamua kumwandikia wimbo unaitwa Ushaniroga,
kuonyesha ni jinsi gani amedata naye.
“Siyo siri jamani ndiyo kashaniroga, nampenda na yeye kaonyesha
upendo wake kwangu, nipo naye na kuhusu huyo Jack Wolper ni maisha tu,
ni rafiki zangu, huwa naona nao katika maeneo tunapiga kiss, ni vitu vya
kawaida lakini sasa niko na Kajala,” alisema.
Hata hivyo, wadada hao wawili wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo hawakuweza kupatikana ili kuzungumzia habari hiyo ambayo ni gumzo ya jiji kwa sasa.
Hata hivyo, wadada hao wawili wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo hawakuweza kupatikana ili kuzungumzia habari hiyo ambayo ni gumzo ya jiji kwa sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni