Kaimu Waziri wa usalama wa ndani wa Ukraine amesema kikosi maalum cha usalama kilicholaumiwa kwa kuwaua waandamanaji kimefutwa.
Arsena Avakov amesema taarifa zaidi kuhusu masuala ya usalama nchini humo zitaendelea kutolewa kwa umma.
Wakati huo huo jamii ya kimataifa imeendelea kugawanyika kufuatia
kuondolewa madarakani kwa Rais Viktor Yanukovych. Waziri wa mambo ya nje
wa Urusi Sergei Lavrov ameomba mataifa kulaani kampeini ya uzalendo
inayoshinikizwa na upande wa Magharibi mwa Ukraine.
Bw Lavrov hasa amekosoa vikali sheria ya kupiga marufuku utumizi wa
lugha ya Kirusi pamoja na tisho la kuwafutia uraia raia wanaozungumuza
lugha hiyo ndani ya Ukraine.Urusi imetaja kuondolewa kwa Yanukovych kama
mapinduzi ya nguvu na imeelezea wasi wasi kuhusu kampeini inayoendeshwa
na mirengo ya kuzalendo inayopinga vikali Urusi.
Ndani ya Ukraine maeneo yanayozungumza Kirusi hasa Mashariki na
Kusini mwa nchi yamepinga kuondolewa kwa Rais Vicktor Yanukovych. Katika
eneo la Crimea wakaazi na utawala wa eneo hilo umepandisha bendera ya
Urusi na kuondoa ile ya Ukraine.
Urusi imesema haitaingilia masuala ya ndani ya Ukraine. Kwa upande
mwingine Marekani na nchi washirika wake Barani Ulaya zinaunga mkono
upinzani na kutambua mamlaka ya sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni