Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu katika Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo, DRC, yamesema kuwa Serikali ya nchi hiyo
itachukuliwa kuwa dhaifu iwapo hamkamati Rais wa Sudan, Omar el Bashir.
Mashirika yapatayo 90 yalitoa wito Serikali ya DRC imkamate el Bashir
ambaye alikuwa mjini Kinshasa kushiriki katika vikao vya muungano wa
COMESA.
Mmoja wa waandalizi wa maandamano ya kushinikiza Serikali imkamate
kiongozi huyo wa Khartoum, Bwana Andre Kito Masimango, amesema:
“kuna barua ambayo inasema kuwa mahali po pote ambapo El Bashiri
anapatikana anapaswa kukamatwa na kupelekwa kwenye mahakama ya
kimataifa.”
Mkerektwa huyo wa haki za kibinadamu anasema kuwa Rais El Bashir
anapaswa kukamatwa kwa heshina ya waathirika wa dhuluma inayodaiwa
kufanywa nchini Sudan na hata DRC yenyewe.
Watu kadhaa ambao wametoa maoni kwenye mtandao wa BBC wamesema kuwa
lilikuwa kosa kwa Serikali ya DRC kumkaribisha Rais El Bashar kwa
mkutano wa COMESA huku ikijua kuwa anatafutwa.
Hata hivyo kuna wale wanaosema kuwa msimamo wa Umoja wa Afrika (AU)
ambao unasema kiongozi anayetawala hapaswi kukamatwa unapaswa
kuzingatiwa ili El Bashir asikamatwe ugenini DRC.
0 comments:
Chapisha Maoni