Jumapili, Februari 02, 2014

HII NDIO AZAM FC

REKODI tatu za klabu na ligi zilivunjwa jana jioni, Azam FC ilivunja rekodi yake ya ushindi mnono baada ya kufunga magoli manne katika mechi moja, idadi hiyo ya magoli ikiwa ni kubwa zaidi msimu huu.
AZam FC ikajiongezea rekodi ya pili ya kushinda mechi muhimu tena ikishinda kwa idadi kubwa ya magoli dhidi ya timu ngumu ya Kagera Sugar. Rekodi ya klbu ya Azam FC tangia kuanzishwa kwake inaonesha kuwa haijawahi kuwa na uwezo wa kushinda mechi inapotakiwa kushinda kwa udi na uvumba ili ikae kileleni.
 Mara ya mwisho ilikuwa ni mechi ya kumaliza raundi ya kwanza ambapo ikiwa nyumbani Azam FC ilipaswa kuifunga Mbeya City ili imalize raundi ya kwanza ikiwa inaongoza lakini ikajikuta ikipata sare ya 3-3.
Rekodi nyingine ambayo ni ya kuvutia zaidi ni ile ya kufikisha mechi ya 16 bila kufungwa. Azam FC imecheza michezo 16, imeshinda michezo 10 na kutoka sare michezo 6 huku ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja hadi hivi sasa.

Katika mchezo wa jana jioni Brian Umony alitakata baada ya kufunga magoli mawili ya awali katika dakika za tisa na 52 huku kinda la miaka 18 Kevin Friday aliyeingia kuchukua nafasi ya Joseph Kimwaga aliyeumia akifunga goli la tatu na Jabir Azizi Stima akikamilisha karamu ya magoli.
Azam FC jana ilikuwa ikicheza mchezo wake wa tatu mkwenye ligi bili kuruhusu nyavu zake kutikisika. Huo ulikuwa ni mchezo wa 12  kwa kocha Marius Joseph Omog bila kuruhusu nyavu zake kuguswa kati ya michezo 13. Aliruhusu kufungwa goli tatu na KCC ya Kampala Uganda Pekee.
Azam FC sasa inajiandaa na mchezo wa kimataifa kukwaana na Club De Ferroviario da Beira mechi itakayochezwa jumapili tarehe 9 February 2014 Chamazi Stadium

0 comments:

Chapisha Maoni