Jumatatu, Februari 03, 2014

CHELSEA YAICHAPA MANCHESTER CITY

TIMU ya Chelsea imeibuka na pointi tatu muhimu katika Uwanja wa Etihad baada ya kuilaza Manchester City bao 1-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England usiku huu.
Bao pekee la Chelsea limewekwa kimiani na Ivanovic dakika ya 32 ya mchezo. Kwa matokeo hayo, Chelsea sasa wana pointi 53 wakiwa nafasi ya tatu huku Manchester City wakiwa nafasi ya pili na pointi 53 wakitofautiana na Chelsea kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Arsenal wanaendelea kubaki kileleni wakiwa na pointi 55 kibindoni baada ya kucheza michezo 24.

0 comments:

Chapisha Maoni