Watu wapatao 11 wamepoteza maisha wakati volcano iliporipuka leo asubuhi huko Indonesia.
Tukio hilo la mlipuko wa volcano limetokea asubuhi ya leo katika mlima Sinabung uliopo kusini mwa Sumatra, Fichuo Tz imepata taarifa hii toka kwa msemaji wa majanga mjini humo aitwaye Sutopo Purwo Nugroho.
Taarifa inaeleza kuwa wahanga waliouawa walipigwa na uji mzito wa moto (magma) uliokuwa ukiripuka kutoka katika mlima huo, na ni wakazi wa kijiji kilicho karibu kabisa na mlima huo.
Waokozi na wachunguzi wanatarajiwa kufika kesho katika eneo hilo kushughulikia janga hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni