Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku
chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuishinisha sheria mpya dhidi ya
mapenzi ya jinsia moja.
Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini
Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia
moja.
Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani
kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja
kwa moja badala ya serikali.
Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.
Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.
Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.
Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.
Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.
Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala,
alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa
zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote
inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.
Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa
Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au
kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.
0 comments:
Chapisha Maoni