![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPL_CfTcMhn1Qz9b7mLLQos88QzlThhjZRk7qmj3xWGnKmGVlWfDDoRaSVw5J0X6608IWxluo9V-vqUO_cZEQz9IdPafByCbjtYLr5ofWVnddaRXpWQ_skNW4N8j1grNt4m_-B8CLc4Om9/s1600/KOMBE-LA-LIGI-KUU-YA-VODACOM-TANZANIA-BARA.jpg)
Ashanti United itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal
Union itacheza na Oljoro JKT katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati
Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya
Azam na Mtibwa Sugar.
Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na
Mgambo Shooting itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex wakati Simba na
Rhino Rangers zitaumana kwenye Uwanja wa Taifa.
Mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine inahamishiwa uwanja mwingine kwa vile huo bado
nyazi zake ambazo zimepangwa hivi karibuni hazijawa tayari kuhimili
mechi hiyo.
Hivyo Tanzania Prisons inatakiwa kutafuta uwanja mwingine unaokidhi
viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mechi hiyo, na nyingine dhidi ya JKT
Ruvu itakayochezwa Januari 29 mwaka huu.
Pia matumizi ya tiketi za elektroniki yanaanza katika mzunguko huu
kwa vile viwanja nane ambavyo tayari vimefungwa vifaa vya tiketi hizo.
Vilevile tunakumbusha washabiki wa mpira wa miguu kuwa tiketi za
elektroniki haziuzwi viwanjani.
0 comments:
Chapisha Maoni