Jeshi la Polisi mkoani Geita, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuiba na kumtorosha mtoto wa miaka sita kwa lengo la kutaka kumdhuru na kumpeleka kusikojulikana.

“Mtoto huyo alichukuliwa kwa baiskeli nyumbani kwa mama yake, Semeni Makoye (25) na mtuhumiwa Makoye na kumpeleka kusikojulikana,” alisema Paulo.
Kamanda alisema kuwa, baadaye Kulwa alirudi nyumbani saa 10 jioni akiwa na mtoto huyo na kudai kuwa alitekwa na watu wanne waliokuwa na gari aina ya Noah.
Aidha, alisema kuwa katika uchunguzi walibaini kuwa mtuhumiwa huyo kabla ya wizi wa mtoto huyo aliwahi kumtongoza mama wa mtoto, lakini baada ya mama huyo kukataa siku chache likatokea tukio la kuibwa mtoto.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Geita, Adamu Sijaona mtoto huyo hakuwa na tatizo lolote baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu kwenye hospitali yake.
“Tumemchunguza mtoto kila sehemu hatukumkuta na tatizo lolote kwenye mwili wake, ila alikuwa na tatizo la ugonjwa wa maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI) ,” alisema mganga huyo wakati akielezea hali ya mtoto.
Katika tukio hilo, mbali na mtuhumi wa kwanza, pia alikamatwa Makungu Panga mwenye miaka 38 mkazi wa Katoro, ambaye ameunganishwa kwenye tukio hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni