Jumatano, Januari 22, 2014

MBUNGE WA CHALINZE AFARIKI DUNIA




Mbunge wa Chalinze, Said Ramadhani Bwanamdogo (CCM) Afariki dunia!!
HABARI zilizotufikia hivi punde ni kwamba Mbunge wa Chalinze, Said Ramadhani Bwanamdogo (CCM), aliyekuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) amefariki dunia!

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi! Amina.

0 comments:

Chapisha Maoni