Jumatano, Januari 22, 2014

DARAJA LA DUMILA LAENDA NA MAJI

Daraja la Dumila mkoani Morogoro lililopo barabara ya Dodoma - Morogoro limekatika na magari hayapiti baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya magari yatokayo upande wa Dodoma na Moro yameamua kugeuza na kurudi yalipotokea maana hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo. Kutokana na mvua hiyo, madarasa katika Shule ya Msingi Magole, Dumila, Morogoro nayo yamefunikwa na maji na wanafunzi kuamua kujiokoa kwa kupita madirishani. Mpaka sasa hali ni tete eneo hilo la Dumila wilayani Mvomero.

0 comments:

Chapisha Maoni