Mahakama ya Ilala, Dar imeridhia kukamatwa kwa gari la
kifahari la Wema Sepetu aina ya Audi Q-7 lenye namba za usajili T 973 BUJ lililokuwa
likiwakosesha akina dada usingizi na kukabidhiwa kwa mmiliki halali kwa
kuwa Wema alikuwa nalo kimagumashi.
Gari hilo limekamatwa Januari 2, mwaka huu Namanga, Oysterbay jijini
Dar likiwa mikononi mwa kijana wa kiume aliyedaiwa kuwa ni mdogo wa
Mbongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’.
“Alikuwa nalo yule dogo ‘waiti’, mdogo wake huyu msanii Diamond.
Alikuwa na wenzake pale Namanga kuna kibarabara cha vumbi, walikuwa
wanarekodi video. Jamaa walikuwa wanalifuatilia so lilipopaki ndipo
wakalipiga ‘tanchi’ (kulikamata),” kilisema chanzo chetu cha kuaminika.
Imefahamika kuwa gari hilo lilikamatwa na kampuni kiboko ya madalali wa
mahakama nchini (court brokers) ya jijini Dar iitwayo Unyangala Auction
Mart Ltd & Court Brokers yenye ofisi zake kwenye Jengo la Harbour
View Tower ‘JM-Mall’, Dar.
Habari za uhakika zilidai kuwa kabla ya kulipeleka ‘yadi’ dogo huyo
aliyekamatwa na gari hilo aliwasiliana na Wema na kumjulisha ambapo
ilisemekana kwamba bidada huyo alichanganyikiwa.
Baada ya pale walilipeleka gari hilo kwenye yadi yao hiyo kisha kuwasiliana na mmiliki halali tayari kwa kumkabidhi.
Baada ya pale walilipeleka gari hilo kwenye yadi yao hiyo kisha kuwasiliana na mmiliki halali tayari kwa kumkabidhi.
0 comments:
Chapisha Maoni