Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo zimetufikia, zinaeleza kwamba watuhumiwa ni jeshi la Polisi, na kwamba walirusha kitu kinachosadikiwa kuwa bomu - lililojeruhi 6, ambapo 4 kati yao wameruhusiwa baada ya matibabu kwenye hospitali ya Mission na ya Wilaya ya Arumeru.Majira ya saa sita na nusu, waumini walidai kuona gari la polisi likipita kwa kasi, na lilipowakaribia walistuka mlipuko ukiwarusha pembeni, ambapo walijikuta na majeraha na usoni, mapajani na maeneo mbalimbali ya mwili. Kisha baada ya hapo gari ilisogea mbele na kuanza kurusha mabomu kwa watu wowote iliokutana nao.
Hadi sasa inaelezwa kuwa uchunguzi umeshaanza kufanyika, huku Kamanda Liberatus Sabas akikataa kuzungumzia zaidi suala hilo. Alipotafutwa na Fichuo Tz, hakueleza kwa kina, lakini akasema kuwa sio suala la kwaya kama ambavyo imeelezwa, bali ni wakinadada wawili na kwamba hawezi kuzungumza zaidi, bali leo (Ijumaa) atatoa taarifa rasmi na iliyo kamili kwa vyombo vya habari.
Alipoulizwa kuwa kama ni kweli jeshi la Polisi linatuhumiwa kuhusika, alisema kuwa atazungumza kesho kuhusiana na tukio hilo. Tukio hili limetokea ikiwa ni siku mbili zimepita tokea kuapishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi mpya, Ernest Mangu ambaye amechukua nafasi ya IGP Said Mwema aliyestaafu.



0 comments:
Chapisha Maoni