Baba mtakatifu Papa Francis ameidhinisha kamati ya
Vatican itakayopambana na visa vya unajisi wa watoto katika kanisa
katoliki pamoja na kuwasaidia waathiriwa kwa kuwapa ushauri nasaha.
Tangazo hili limelotolewa na naibu askofu mkuu
Sean O'Malley mjini Boston Marekani, na linakuja baada ya kufanyika
mkutano kati ya Papa na makadinali wake wanane ambao humshauri.
Kadhalika tangazo lenyewe linakuja
baada ya Vatican kukataa ombi la Umoja wa Mataifa la kutaka ukabidhiwe
taarifa za kanisa hilo kuhusu madai ya makasisi na watawa wanaodaiwa
kuwanajisi watoto.
Papa Francis, amesema kuwa swala la kukabiliana
na visa vya makasisi kuwanajisi watoto ni muhimu sana ili kuweza
kulirejeshea hadhi kanisa Katoliki.
Kadinali, Sean O'Malley, naibu askofu mkuu wa
kanisa hilo mjini Boston, alisema kuwa kamati hiyo inaweza kutoa
mwongozo wa kikazi kwa makadinali na maafisa wa kanisa ili kulainisha
utenda kazi wa viongozi wa kanisa.
Mji wa Boston ndio ulikuwa kitovu cha madai ya makasisi kuwanajisi watoto nchini Marekani mwaka 2002.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, naibu
Askofu alisema kuwa kamati hiyo mpya ilipendekezwa na baraza la
makadinali, ambalo lilibuniwa ili kufanyia mageuzi kanisa katoliki. Papa
aliliidhinisha Alhamisi.



0 comments:
Chapisha Maoni