Miaka 146 iliyopita katika siku kama ya leo Madam Escudo Doska ambaye
baadaye alikuwa maarufu kwa jina la Marie Curie alizaliwa huko Warsaw
mji mkuu wa Poland.
Baba yake alikuwa profesa wa fizikia na baadaye
Madam Curie pia alielekea Paris Ufaransa kwa ajili ya kuendeleza masomo
yake katika taaluma hiyo hiyo kama alivyofanya baba yake.
Hatimaye
mwanamama huyo alifanikiwa kuvumbua mada ya radium baada ya utafiti na
kutwalii kwa miaka mingi. Ni vyema kuashiria hapa kuwa Madam Curie
alitunukiwa tuzo ya Nobel mara mbili katika taaluma za fizikia na kemia
na aliaga dunia mwaka 1934.
Na siku kama ya leo miaka 57 iliyopita vita vya mfereji wa Suez
vilimazika baada ya Umoja wa Mataifa kuingilia kati. Vita hivyo vilianza
baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia jangwa
la Sinai na kufuatia mashambulizi ya askari wa miavuli wa Uingereza na
Ufaransa katika eneo la mfereji huo.
Serikali hizo tatu zilianzisha vita
hivyo kufuatia hatua ya rais wa wakati huo wa Misri Gamal Abdulnassir
ya kuutaifisha mfereji wa Suez.



0 comments:
Chapisha Maoni