Leo ni Jumatatu tarehe 29 Mfungo Tatu Dhulhija mwaka 1434 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 4 Novemba mwaka 2013 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 49 iliyopita, askari vibaraka wa
utawala wa Shah uliokuwa ukitawala nchini Iran waliivamia nyumba ya Imam
Khomeini muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Qum na kumtia
mbaroni. Baada ya kumhamishia mjini Tehran utawala wa Shah ulimbaidishia
Imam Khomeini nchini Uturuki. Utawala wa Shah uliamua kufanya hivyo
kutokana na uungaji mkono wake kwa harakati za mapambano za wananchi wa
Iran za kutaka kuung'oa madarakani utawala huo. Lengo la kumbaidisha
kiongozi huyo wa kidini, kisiasa na mwanamapinduzi, lilikuwa ni
kusimamisha harakati za kiongozi huyo pamoja na mapambano ya wananchi
Waislamu wa Iran dhidi ya utawala huo.
Siku kama ya leo miaka 67 iliyopita, Shirika la Elimu,
Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, liliasisiwa kwa
ushirikiano wa nchi 43. Lengo la kuasisiwa taasisi hiyo lilikuwa ni
kuanzisha mawasiliano ya kielimu na kiutamaduni baina ya mataifa
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusambaza vitabu na makala kwa lugha
mbalimbali duniani. Miongoni mwa nukta muhimu za kuvutia zilizoko katika
hati ya UNESCO ni haja ya watu wote kuheshimu uadilifu, utawala wa
sheria na kulinda haki za binadamu pamoja na uhuru wa mwanadamu. Katibu
Mkuu, Kamati ya Utendaji na Vikao vya Baraza Kuu ndizo nguzo muhimu tatu
za kimsingi za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa
Mataifa.
Na miaka 18 iliyopita kama leo, Is'haq Rabin Waziri Mkuu wa
zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel aliuawa na Mzayuni mwenye
misimamo ya kufurutu ada. Is'haq Rabin alifanikiwa kuwa Waziri Mkuu wa
Israel kuanzia mwaka 1974 hadi 1977 kwa tiketi ya Chama cha Leba. Hata
hivyo aliuzuliwa wadhifa huo kwa tuhuma za ubadhirifu. Ni muhimu
kukumbusha kuwa, Is'haq Rabin alikuwa mingoni mwa makamanda wa makundi
ya kigaidi ya Kizayuni.



0 comments:
Chapisha Maoni