Jumapili, Novemba 17, 2013

AKATWA MGUU NA MUMEWE, ASHINDWA KURUDI NYUMBANI KISA MAHARI ALIYOTOLEWA

Hali ya wanawake inazidi kuwa mbaya ndani ya nchi yao TANZANIA inayosifiwa kuwa ni Kisiwa cha Amani (Amani kwa wanaume) Tukio hili lilitokea mapema mwezi wa nane mwaka huu Kijiji cha Nyantira Tarime Mara. Katika mazungumzo yake huyu binti alisema kwamba anatamani sana kurudi nyumbani kwa wazazi wake, tatizo ni kwamba kwa kuwa alilipiwa MAHARI na mume wake (aliyemkata panga mguu na kuutoa) hawezi kurudi kwao , wala mama yake hawezi kumkubalia arudi kwao ni mpaka baba yake aje atoe ruhusa ya yeye kurudi nyumbani au abaki kwa mume muuaji avumilie-MFUMO DUME UMEKAMATA MIZIZI (mbayaaaaa, sanaaaa. anajisemeaga Mch Rwakatare)

Samahani kwa picha mbaya, lakini hatuna budi kuonyesha unyama uliopita kipimo ambao wanawake wanaupitia. Na huu ni mfano halisi kwa mwanamke huyu wa Tarime Musoma. picha ya juu ni kipande cha mguu wa huyo binti ambao mume alipitisha panga mithili anakata muwa, picha inaonyesha mguu uliobaki na mguu wa kushoto pia ulikatwa lakini haukutoka, pamoja na mkono wake wa kushoto ulikatwa lakini haukutoka. ( Kumbuka tupo kwenye maandalizi mazito ya kuandimisha siku 16 za kupinga ukatili dhili ya Wanawake)

0 comments:

Chapisha Maoni