Maafisa wa Ufilipino wameripoti kuwa watu wasiopungua 93 wamefariki dunia na mamia ya wengine kujeruhiwa kufuatia mtetemeko wa ardhi ulioyakumba maeneo ya katikati mwa nchi hiyo. Kitovu cha zilzala hiyo iliyokuwa na ukubwa wa 7.2 kwa kipimo cha rishta kilikuwa huko kusini-kusini mashariki mwa Manila, mji mkuu wa Ufilipino karibu na Catigbian. Ofisi ya gadi ya rais wa Ufilipino imetangaza kuwa mamia ya watu wengine wamejeruhiwa baada ya zilzala hiyo kuangusha majengo, mapaa ya nyumba na kuharibu barabara katika visiwa vya Bohol na Cebu.
Mwezi Februari mwaka 2012 watu zaidi ya mia moja waliaga dunia na wengine kutoweka baada ya mtetemeko wa ardhi uliokuwa na ukubwa wa 6.9 kwa kipimo cha rishta kukikumba kisiwa cha Negros huko Visayas.



0 comments:
Chapisha Maoni