Shirika la Umoja wa Mataifa limesema kuimarishwa kwa ulinzi
wa kutumia meli Somalia kumesaidia kupunguza wimbi la mashambulizi ya maharamia
nchini humo.
Ripoti ya Katibu mkuu wa Umoja huo, Ban Ki-Moon, imeonyesha kuwa kumetokea
mashambulizi 17 tu mwanzoni mwa mwaka huu, ikilinganishwa na mashambulizi 99
yaliyofanywa mwaka jana mwanzoni.
Mpaka Oktoba 17 mwaka huu ni meli moja tu ndogo yenye abiria 60 ambayo bado inashikiliwa na maharabia, wengi wao wakiwa hawajulikani na maharamia hao kuendelea kuneemeka ambapo mwaka jana walikusanya hadi bilioni 40 za Marekani kama fidia ya kuwaachia huru mateka.
Huku hayo yakiendelea na Somalia ikifanya mchakato wa kujijenga upya baada ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na kile kinachoelezwa kuwa mfumo mbaya wa sheria tangu kupinduliwa madarakani kwa Rais Siad Barre wa nchi hiyo mwaka 1991, Umoja wa Mataifa umetaka kuimarishwa zaidi kwa ulinzi.
Hata hivyo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ripoti hiyo amelaumu kitendo cha maharamia hao kuwateka kwa muda mrefu na kuwatesa watu wasio na hatia na kuwatishia ikiwa hawataweza kutoa kiasi kikubwa cha fedha wanachotozwa ili kuachiwa huru.



0 comments:
Chapisha Maoni