Anasema mpaka kufikia Septemba 20, 2013,
wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 9,283 toka nchi za Rwanda, Burundi,
Uganda, Somalia, DRC Congo, Yemen na India, kwa madai ya kuishi nchini
isivyo halali.
Zamaradi anasema kilichomsukuma Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuanzisha operesheni hiyo ni
kukithiri kwa matukio ya uhalifu hasa katika mikoa iliyopo pembezoni mwa
nchi.
“Operesheni Kimbunga ilianzishwa kwa lengo la
kukabiliana na vitendo vya uhalifu vilivyokithiri vikiwemo ujambazi wa
kutumia silaha,ujangili, utekaji wa magari na mauaji ya kikatili pamoja
na migogoro ya ardhi inayotokana na wafuagaji kutoka nchi jirani
kuingiza mifugo yao kwa ajili ya malisho,” anasema Zamaradi.
Aidha amesema idadi kubwa ya wahamiaji haramu
waliokamatwa ni kutoka Burundi (5,355) wakiafuatiwa na Rwanda (2,379),
Uganda (939), DRC Congo (564), Somalia (44), Yemen (1) na India (1).



0 comments:
Chapisha Maoni