Jumatatu, Septemba 09, 2013

SIKU YA LEO KATIKA HISTORIA

Siku kama ya leo miaka 37 iliyopita, alifariki dunia Mao Tse Tung kiongozi wa Jamhuri ya Watu wa Uchina. Tse Tung alizaliwa mwaka 1893 na mwaka 1921 aliunda Chama cha Kikomonisti akiungwa mkono na wanafikra wenzake. 
Mao Tse Tung alikuwa akihitilafiana na baadhi ya mitazamo ya Marxi na Lenin, sababu iliyopelekea fikra zake hizo kujulikakama kama fikra za Maonisim.

Siku kama ya leo miaka 814 iliyopita, alizaliwa Ibn Muniir, faqihi na mfasiri wa Qur'ani Tukufu katika mji wa Alexandria nchini Misri. Baada ya kujipatia elimu ya msingi kutoka kwa baba yake, Ibn Munir alijiendeleza kielimu kutoka kwa maulamaa wengine na kufikia daraja la juu kielimu. Ibn Muniir katika kipindi cha uhai wake, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ukiwemo Ukadhi. Alifariki dunia katika mji wa wa Alexandria na kuzikwa kwenye msikiti maarufu unaojulikana leo hii kwa jina la Masjidu Jame'e al Muniir.

Na miaka 12 iliyopita katika siku kama ya leo, Ahmad Shah Masoud, mmoja wa makamanda wakuu wa Mujahidina wa Afghanistan aliuawa. Ahmad Shah Masoud alizaliwa mwaka 1952. 
Masoud alianza kupigana vita na vikosi vya kigeni katika maeneo ya milimani ya kaskazini mwa Afghanistan, sambamba na kuingia madarakani nchini humo utawala wa kikomonisti mwaka 1979. Muda mfupi baadaye Afghanistan ilikaliwa kwa mabavu na jeshi la Urusi ya zamani.

0 comments:

Chapisha Maoni