Jumanne, Septemba 10, 2013

OPARESHENI YA KIKWETE YAZAA MATUNDA


Oparesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu, kuwakamata watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, imeanza kuzaa matunda ambapo bastola 38 na bunduki za kivita zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uhalifu, zimerejeshwa polisi.
Kurejeshwa kwa silaha hizo kumetokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa hivi karibuni akiwataka wahamiaji haramu kurejea katika nchi zao ndani ya wiki mbili na watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wazisalimishe
Akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu kuhusu operesheni hiyo iliyoanza Agosti mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma, Bw. Venance Mwamotto, amesema operesheni hiyo ambayo ni endelevu, imelenga kukomesha vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha mkoani humo.
Aidha amesema operesheni ya salimisha silaha kwa hiari na utoaji siri za watu wanaojihusisha na matukio ya uhalifu, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi mkoani humo, wananchi na viongozi wa mkoa huo.
Pia amesema kuwa hadi sasa bastola zilizosalimishwa ni 38 na bunduki za kivita SMG ni mbili, moja imepelekwa katika Kituo cha Polisi Kibondo na mwanamke, Bi. Erica Josamu (35), mkazi wa Kibondo. Kati ya watu waliorejesha silaha hizo zinazoweza kutumika kwenye vita ni mmoja ambaye ameonesha ujasiri, nao hatukusita kumzawadia kwa hiari.
Ameongeza kuwa , katika mahojiano ya awali na mwanamke huyo, amesema silaha hiyo aliiokota njiani na kuamua kuifikisha kituoni hapo, lakini baadaye alikiri kuimiliki na kuitumia kinyume cha sheria na hakuchukuliwa hatua zozote.
Bw. Mwamoto amesema wamefanikiwa kuokota silaha nyingi zilizotupwa na wananchi hasa maeneo ya Kambi ya Nduta, ambayo walikuwa wakiishi wakimbizi ambapo eneo hilo lilikuwa maficho ya majambazi sugu.Amesema maeneo mengine yaliyookotwa silaha ni Kamuhasha, Kumbanga na Kanembwa ambapo kulikuwa na matukio mengi ya uhalifu wa kutumia silaha.

0 comments:

Chapisha Maoni