Jumanne, Septemba 10, 2013

MEMBE AOMBA RHADHI KWA WANANCHI JIMBONI KWAKE

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe, amewaomba radhi wananchi wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi kwa kutoonekana jimboni kwake muda mrefu.
Amesema hali hiyo imechangiwa na majukumu aliyonayo kitaifa, kimataifa na kuahidi kutumia muda wa likizo kufanya ziara katika jimbo hilo ili aweze kuzungumza na wananchi.
Bw. Membe ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ili kumpata Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) wa chama hicho, uliofanyika kwenye Kata ya Kiwalala, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi.
Amesema majukumu aliyoongezewa serikalini, yamechangia kwa kiasi kikubwa kutofika jimboni kwake mara kwa mara hivyo hutumia muda mwingi kutekeleza majukumu hayo 
Amesema yeye ataendelea kuwapenda wapigakura wake ambao ndio waliompa dhamana ya kuwa mbunge wao hivyo kitendo cha kutoonekana kutoonekana kwake jimboni kusiwanyong'onyeze.

0 comments:

Chapisha Maoni