Madiwani wa halmashauri ya jiji la Mbeya kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamesusia kikao cha kamati ya fedha na utawala kutokana na kuwa na mashaka ya mapendekezo ya kamati hiyo.
Amesema licha ya kucheleweshwa kwa hoja hizo mwenyekiti wa mkutano huo hakuwatendea haki madiwani wa CHADEMA kwa kauli yake ya kusema wengi wape sababu iliyowapelekea madiwani wa CHADEMA kushindwa kutoakana na uchache wao hatimaye kuamua kutoka nje.
Kwa upande wa mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga amesema kitendo walichofanya wabunge wa CHADEMA cha kususia kikao hicho ni kinyume na sheria na watachukuliwa hatua.



0 comments:
Chapisha Maoni