Jumamosi, Agosti 10, 2013

MUME AMLAWITI MWANAE NA KUMBAKA SHEMEJI YAKE

Bw  Mohammed, mkazi wa Kigamboni jijini Dar amedaiwa kuwafanyia unyama watoto wawili, akimlawiti mwanaye wa kufikia na kumbaka mdogo wa mkewe.


Akizungumza na mtandao huu juzi nyumbani kwake, mke wa mtuhumiwa huyo, Zubeda alisema watoto waliofanyiwa hivyo ni mwanaye wa kiume (6) na mdogo wake wa kike (16) (majina tunayo).
Mwanamke huyo alisema: Nilikutana na Mohammed nikiwa na mtoto huyo wa kiume, ndani  ya uhusiano wetu tukajaliwa kupata mtoto wa kiume hivi karibuni, hapo ndipo matatizo yalipoanza.
“Alihama chumba ili mimi nilale na kichanga, akaenda kulala na mtoto huyo. Niliamini angemchukulia kama mwanaye kwa kuwa tulishaoana.
“Mwaka jana alikuja mdogo wangu, tukabadili kulala, tuliwaacha watoto hao walale chumba kimoja mume wangu akarudi chumbani. Alizua tabia ya kutoka usiku eti kuvuta sigara kumbe alikuwa anakwenda kumwingilia mdogo wangu,” alizidi kudai mwanamke huyo.
Alidai kuwa ikafika wakati akagundua mwanaye huyo anajisaidia kwenye nguo na kinyesi kinakuwa na damu, akawa anampiga na kumwamuru afue nguo mwenyewe.
“Juzi shoga yangu mmoja alikuja akaniambia amemsikia  mume wangu akitamba baa kwamba amemtoa ‘usichana’ mdogo wangu.
“Nilimuuliza mtoto wangu ambapo aliniambia ni kweli baba yake amekuwa akienda chumbani kwao na kumfanyia mchezo mbaya.
“Ukweli taarifa hizo zilinishtua sana, sikutarajia mdogo wangu kama angeweza kulala na mume wangu, nilimpiga sana.
“Wakati namwadhibu mtoto wangu naye akaona kumbe kitendo kile ni kibaya akasema hata yeye baba yake amekuwa akimfanyia mchezo mchafu kila siku usiku,” alisema mama huyo huku akilia.
Wakati watoto hao wakikiri kufanyiwa hivyo, Mohammed alikuwa akiwasikia na kujitetea kwamba walikuwa wakimsingizia, ghafla alipokea simu na kusema anakwenda kwenye biashara akirudi watazungumzia suala hilo lakini hakurudi tena mpaka habari hii inapoandikwa.
Baada ya kuona hivyo, mke huyo alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni na kufungua kesi mbili zenye namba KGD/RB/5218/2013 KUBAKA na KGD/RB/5244/2013 KULAWITI, mpaka sasa mtuhumiwa huyo anasakwa na polisi.
Mwanamke huyo alisema alipewa PF3 na kuwapeleka waathirika hao Hospitali ya Vijibweni na vipimo vilionesha waliharibiwa sehemu zao za siri.
Mama huyo alisema daktari amemwambia mtoto wake wa kiume angeweza kupoteza uhai kama
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mwema, Mwinyi Baishe alithibitisha kusikia madai hayo.
angeendelea kufanyiwa mchezo huo.

0 comments:

Chapisha Maoni