Jumatatu, Agosti 07, 2017

AMBALO HUKULIFAHAMU NI KUHUSU NOTI YA PESA KUTENGENEZWA KWA PAMBA

Kutokana muonekano wake unaweza dhani ni karatasi maalumu, ama kuna nakshi nyingine huongezwa ili kuifanya noti iwe nzuri na imara, wakati mwingine yenye kuvutia zaidi, lakini ukweli ni kwamba noti ya pesa hutengenezwa kwa matirio ya aina mbili, karatasi na pamba.
Pamba ninayoizungumza hapa ni ileile ilimwayo kanda ya ziwa, hii katika matengenezo ya noti huwekwa kwa asilimia 75% wakati karatasi yenyewe ikitumika kwa 25% tu.
Watengenezaji wa pesa wamelenga kuifanya noti kuwa kuwa imara, na kupunguza uwezekano wake wa kuchakaa mapema na ndio maana ukiitazama noti ya pesa haswa ikiwa mpya ni kapa plastiki hivi, lakini huwa ni wingi wa pamba ambao huchangia kupata muonekano huo.
Leo umefahamu kuhusu hili kupitia Fichuo, karibu wakati mwingine ufahamu mengine zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni