Zanzibar imezindua kampeni ya usafi kwenye vijiji viwili vya utalii, ili kuhimiza sekta ya utalii visiwani humo. Kampeni hiyo iitwayo "Best of Zanzibar" inashirikisha wataalamu wa afya kutoka chuo kikuu cha Zanzibar SUZA, na itatekelezwa kwenye eneo la kaskazini mwa kisiwa cha Unguja, kwa lengo la kuchochea ukuaji wa utalii, baada ya utafiti kuonesha kuwa ukosefu wa usafi umeathiri wakazi na watalii kwenye eneo hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni