Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi imesaini mikataba yenye zaidi ya Tsh. Bilioni moja na wakandarasi wa Barabara kwa lengo la kuzifanyia matengenezo baadhi ya barabara zilizo chini ya halmashauri hiyo, zikiwa na urefu wa takaribani km 151.
Taarifa ya Afisa habari na mawasilino wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imetanabaisha kuwa, halmashauri imeingia mikataba na makampuni 11 ikiwa na thamani ya Tsh. Bilioni 01, milioni kumi, laki 05 na elfu tatu miamoja na 24.
Mwakapiso, amezitaja baadhi ya barabara zitakazofanyiwa matengenezo kuwa ni pamoja na barabara ya Kilosa Mufindi matengenezo ya nara kwa mara km12, mpangatazara- Mlimba km 21, Ihalimba- Igomtwa na usokami km 11 wakati ile ya Iramba – Ipilimo itatengenezwa kwa urefu wa km 13.
Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi inamajimbo mawili ya uchaguzi yenye mtandao mzuri wa barabara km 1,000.6 ambazo halmshauri imekuwa ikizifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuziwezesha zipitike misimu yote ya mwaka kwa kuzingatia kuwa uwepo wa shughuli za viwanda na mazao ya misitu hususani mbao husababisha barabara hizo kutumika sana kwani mapema mwezi disemba mwaka jana ilisaini mikataba 10 yenye thamani ya milioni 500.
0 comments:
Chapisha Maoni