Jumatano, Machi 01, 2017

WACHINA KUJENGA KIWANDA CHA SARUJI TANZANIA

Serikali ya Tanzania imepongeza uamuzi wa wawekezaji wa China kujenga kiwanda kikubwa cha saruji katika mkoa wa Tanga kaskazini mashariki wa Tanzania. 
Kiwanda hicho kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
Waziri Mkuu wa Tanzania Bw Kassim Majaliwa amesema kujengwa kwa kiwanda hicho kutakuwa na maana kuwa Tanzania, kwa kuwa kitakidhi mahitaji ya saruji na kuifanya ipatikane kwa bei nafuu.
Bw. Majaliwa pia amesema ujenzi wa kiwanda hicho utachochea maendeleo ya viwanda, pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Mkuu wa Kampuni Sinoma Bw Peng Jianxin amesema uwekezaji kwenye kiwanda hicho utakuwa na awamu mbili, na awamu ya kwanza itagharimu dola bilioni moja za kimarekani.

0 comments:

Chapisha Maoni