Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hii leo ameefanya uteuzi kwa kumteua Mhe. Mama Salma Kikwete kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mama Salma Kikwete ni mke wa aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Salma Kikwete ambaye kitaaluma ni mwalimu ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 comments:
Chapisha Maoni