Jumamosi, Machi 11, 2017

VIGOGO WA CCM WALIOTIMULIWA UANACHAMA NA WALIOPEWA ONYO HAWA HAPA

Habari  kutoka Dodoma, zinaeleza kwamba mwanachama mkongwe wa CCM, Sophia Simba amevuliwa uanachama wa chama hicho huku wanachama wengine ambao ni Emmanuel Nchimbi na Adam Kimbisa wakipewa onyo kali.
Habari zinazidi kueleza kuwa chanzo cha Simba kuvuliwa uanachama na wenzake kupewa onyo, ni madai ya kukisaliti chama, hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2015.
Habari zaidi zinaeleza kuwa wengine waliofukuzwa uanachama ni Ramadhan Madabida, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga. Habari zaidi zitaendelea kukujia kupitia hapahapa.

0 comments:

Chapisha Maoni