Jumamosi, Machi 11, 2017

ZAMBIA KULIMA BANGI KWAAJILI YA TIBA

Nchi ya Zambia inafikiria kuanza kilimo cha bangi kwa ajili ya matibabu kufuatia ufunuo wa serikali kwamba sheria za nchi hiyo zinaruhusu.
Waziri wa Mambo ya Ndani Stephen Kampyongo alisema kwamba kilimo cha bangi kwa ajili ya matibabu inaruhusiwa lakini wale walio na madhumuni ya kujitosa katika biashara hii wanapaswa kupata leseni kutoka kwa Wizara ya Afya.
Katika taarifa ya mawaziri katika bunge kufuatia ongezeko la wito kwa serikali kuhalalisha kilimo cha bangi kwa ajili ya matibabu,waziri alisema kuwa bado ni kosa kwa mtu yeyote kufanya kilimo cha bangi,hata kwa ajili ya matibabu ikiwa hana leseni.

0 comments:

Chapisha Maoni