Jumanne, Machi 07, 2017

SAIDA KAROLI: DIAMOND, BELLE 9 NA DARASSA WAMENIRUDISHA KWENYE RAMANI YA MUZIKI

Mwanamuziki wa zamani wa nyimbo za asili kutoka mkoani Kagera, Saida Karoli aliyepotea kwa kipindi kirefu sasa ametoa heshima na shukrani kubwa kwa wanamuziki wa kizazi kipya ama Bongo Fleva Diamond Platumz kutoka WCB, Belle 9 na rapa Darassa kwa kurudia nyimbo zake kwani kwa kufanya hivyo amerejeshwa katika ramani ya muziki Tanzania.
Saida Karoli ambaye ni mama wa watoto 5 na ufahamu kuwa alianza kuitwa mama akiwa na umri wa miaka 13 tu amekiri kupotezwa na watu wa awali waliommanage kwakuwa hakujua kusoma na kuandika kipindi hicho hivyo hata mikataba aliyoingia kipindi hicho haikuwa na tija kwake na aliishia kudhulumiwa.
Akizungumzia ujio wake mpya Saida anatuambia kuwa kwasasa yuko kamili na kati ya watu wa awali anaotaka kushirikiana nao katika game ya muziki ni wale waliorudia nyimbo zake na kutaka sasa wazirudie pamoja ili kutengeneza ladha mujaarabu, hawa ni Diamond, Belle 9 na Darassa

0 comments:

Chapisha Maoni