Jumanne, Machi 07, 2017

ARSENAL WAPIGWA 10-2, NAPOLI NAO WALIZWA NA REAL MADRID

Arsenal walibomolewa na Bayern Munich kwa mara nyingine tena na kujikuta wakitolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya katika ngazi ya timu 16 kwa kuzabwa jumla ya magoli 10-2.
Arsene Wenger, ambaye atakuwa chini ya shinikizo kali kufuatia kichapo hiki, alishuhudia timu yake ikifungwa magoli 5-1, baada ya kuongoza kwa kupitia bao lililofungwa na Theo Walcott katika kipindi cha kwanza.
Mchezo ulibadilika baada ya Laurent Koschielny kumvuta Robert Lewandowski katika eneo la hatari na kusababisha penati, mapema kipindi cha pili. Koschienly pia alioneshwa kadi nyekundu baada ya mwamuzi kubadili mawazo kufuatia kumuonesha kadi ya manjano awali.
Baada ya hapo mafuriko yalianza, yakiongozwa na Arjen Robben, akifuatiwa na Douglas Costa na Arturo Vidal aliyefunga mabao mawili.
Katika mchezo mwingine wa ngazi ya timu 16, Sergio Ramos alipachika mabao mawili na kuipatia ushindi Real Madrid wa mabao 3-1 waliokuwa wakicheza ugenini dhidi ya Napoli.
Vijana hao wa Zinedine Zidane walishinda kwa jumla ya mabao 6-2 na kujihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali. Alvaro Morata alifunga bao la tatu la Real Madrid.

0 comments:

Chapisha Maoni