Alhamisi, Machi 09, 2017

ALIYETOA DAWA ZA KULEVYA TANZANIA AHUKUMIWA KIFUNGO JELA MIAKA 6 UINGEREZA

Mwanaume mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na miezi minne jela nchini Uingereza kwa kosa la kujaribu kuingiza nchini humo kilo 6.76 za heroin zenye dhamani ya Pounds 600,000 kutoka Tanzania.
Adam Kamaizi Wimana (46) ambaye ni raia wa Uingereza anayeishi Peel Court, Slough alikiri kosa lake. Pamoja na kifungo hicho, mahakama imetoa amri kwa Adam Kamaizi Wimana kutosafiri nje ya Uingereza kwa muda wa miaka miwili baada ya kumaliza kifungo chake.
Bw. Wimana (46), alikamatwa Januari 11, 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow (Terminal 4) baada ya kutua na ndege kutokea Nairobi. Bw. Wimana alipanda ndege Nairobi baada ya kusafiri na mzigo huo akitokea Zanzibar, Tanzania.
Maafisa wa Heathrow walikagua moja ya mabegi yake na kungudua kuwa lilikuwa zito hata baada ya kutoa vitu vyote. Walipochunguza zaidi ndo wakakuta heroin imefichwa juu na chini ya begi hilo.

0 comments:

Chapisha Maoni