Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Felix Simbu ameibuka mshindi na kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya riadha ya dunia ya Mumbai Marathoni yaliyofanyika nchini India.
Simbu ametumia masaa 2 dakika 9 na sekunde 32, na kuwapiku Joshua Kirkorir wa Kenya aliyeshika nafasi ya pili aliyetumia saa 2, dakika 9 na sekunde 50 na Eliud Barbgetuny wa Kenya alishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 2 dakika 10 na sekunde 39.
Akizungumzia ushindi huo, Simbu amesema siri kubwa ya ushindi wake katika mbio hizo ni mazoezi aliyoyafanya katika milima mbalimbali ya Tanzania, yaliyomfanya awe imara zaidi katika mazingira ya mashindano hayo yalikuwa yanakabiliwa na kona pamoja na vilima vingi
Jambo lingine lililomsaidia ni uzoefu alioupata katika mashindano mengine ikiwemo Olimpiki za mwaka jana na mashindano ya ubingwa wa dunia ya Beijing mwaka 2015.
Simbu anakumbukwa pia kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania vyema katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika nchini India mwaka jana kwa kukamata nafasi ya tano katika mbio za marathoni
0 comments:
Chapisha Maoni