Jumapili, Mei 29, 2016

VIBOKO NA FAINI UKIPATIKANA UMEVAA NGUO FUPI TANZANIA

Wanawake katika eneo la Siha Kilimanjaro Tanzania wanaovaa vinguo vifupi watakiona chamtema kuni baada ya usimamizi wa kijiji kupitisha adhabu ya viboko 15 na faini ya shilingi elfu 50 .
Fauka ya hayo mwanamume yeyote ataefumaniwa katika kumbi za starehe za mtoto wa chini ya umri wa miaka 18 aidha atakabiliwa na adhabu hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Sanye Moses Mnuo anasema hizi ni harakati za kupunguza maovu.

0 comments:

Chapisha Maoni