Jumamosi, Mei 28, 2016

CHANJO YA UKIMWI KUJARIBIWA KWA KIASI KIKUBWA NCHINI AFRIKA KUSINI

Taasisi ya Mzio na Maradhi ya kuambukiza ya taifa ya Marekani imetangaza kuwa itafanya jaribo kubwa la ufanisi wa mchanganyiko wa chanjo ya UKIMWI nchini Afrika Kusini.
Mchanganyiko huo ni pamoja na chanjo ya kuchochea mfumo wa kinga na chanjo nyingine ya kuongeza uwezo wa kinga. Mwaka 2009 jaribio lililofanywa huko Thailand limeonesha kuwa, chanjo hiyo inaweza kupunguza hatari ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI kwa asilimia 31. Baada kuboresha chanjo hiyo, wanasayansi walifanya jaribio dogo la awali huko Afrika Kusini, ambalo matokeo yameonesha chanjo hiyo ni salama.
Taarif iliyotolewa na Taasisi hiyo imesema, jaribio kubwa litafanywa mwezi Novemba katika sehemu 15 nchini Afrika Kusini, ambalo litashirikisha watu wazima 5,400 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 walioko kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa na UKIMWI. Kila mshiriki atachanjwa chanjo au placebo mara tano katika mwaka mzima. Matokeo yanatarajiwa kutangazwa nusu ya pili ya mwaka 2020.

0 comments:

Chapisha Maoni