Jumapili, Mei 29, 2016

BAADA YA TAIFA STARS KUTOKA SARE KENYA LEO, TFF WAMEYASEMA HAYA:

Msomaji wetu leo umechezwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania palepale nchini Kenya. Katika mchezo huo matokeo yalikuwa ni sare ya goli 1-1 baada ya Elias Maguli kuanza kuifungia Taifa Stars dakika ya 32 ya mchezo na kisha Victor Wanyama kusawazisha Harambee Stars kwa penalti. Sasa baada ya mchezo huo, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF wameyasema haya; 
"Maoni yetu yanapokelewa. Wito wa TFF ifike mahali tumwache Kocha kama walivyo kwa makocha wengine, waamue. Hivi leo ni wangapi walimpinga Van Gaal kuhusu kumchukua kinda, Rishford. matokeo yake nini? tumpe fursa mwalimu. Tukiamua kwa sasa kila mmoja alete wacheza au timu yake. Stars itakuwa na wachezaji zaidi ya 1,000. Ameita 27, kulingana na uwezo amesafiri na 24 na ndio hao anapambana nao.
Matokeo ya leo ni sare ya 1-1. Elias Maguli alianza kuifungia Tanzania bao katika dakika ya 32 ya mchezo ambao Stars wakati wote ilikuwa inapata sapoti ya mashabiki wake waliokuja Kenya kutoka Tanzania.
Krosi safi ya beki wa kulia Juma Abdul Jafari ndiyo iliyotua kichwani mwa Maguli na kufunga bao hilo lisilo na mawaa. Victor Wanyama, nyota wa Kenya anayecheza klabu ya Southampton ya England, ndiye aliyeisawazishia Kenya, tena kwa bao la penalti baada ya Abdul kumkwatua mmoja wa wachezaji wa Kenya katika harakati za kuokoa hatari langoni kwa Stars.
Kocha amefarijika, kila mmoja amefuraji kwa Tanzania kung'ara ugenini. Nini alichozungumza Kocha Charles Boniface Mkwasa, baada ya muda nitakuletea neno kwa neno kadiri nilivyomnukuu wakati anazungumza na waandishi wa habari wa Kenya na Tanzania. endelea kufuatilia. Tumpe sapoti Mkwasa, tuipe Sapoti taifa Stars, inaweza na mwakani tunaweza kwenda kucheza AFCON."

0 comments:

Chapisha Maoni