Jumanne, Aprili 19, 2016

KUONGEA NA SIMU KUPITA KIASI HUSABABISHA SHINIKIZO LA DAMU

Watafiti wa Italia wametoa ripoti inayosema kwamba, baada ya kuchunguza wagonjwa 94 wenye shinikizo la juu la damu, waligundua kuongea kupitia simu za mkononi kunaweza kuongeza shinikizo la damu.
Kwenye jaribio la kutafuta uhusiano kati ya simu ya mkononi na shinikizo la damu, watafiti waliwafanya washiriki wa jaribio kukaa katika kiti chumbani na kupimwa shinikizo la damu kila baada ya dakika moja, kwa ujumla mara 12. Halafu watafiti waliwapigia simu kwa mara zaidi ya 3.
Matokeo ya jaribio yameonesha kuwa wagonjwa hao wanapoongea kupitia simu za mkononi, shinikizo la damu lao ni juu kuliko wakati hawaongei kupitia simu za mkononi, lakini kiwango cha moyo hakiathiriwa.
Hivyo watafiti waliwashauri watu wenye shinikizo la damu la juu wanapopimwa shinikizo hilo, wasitumie simu za mkononi, ili kuhakikisha usahihi wa matokeo ya upimaji.

0 comments:

Chapisha Maoni